Wajasiriamali Wanawake 600 Wapata Mikopo Isiyo na Riba
Na Ferdinand Shayo,arusha.
Serikali mkoani Arusha kwa kushirikiana na wafanyabiashara, wametoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya milioni 120 Kwa wajasiriamali wadogo wanawake 600 hatua ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Waziriwa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,AjiranaWalemavu Jenister Muhagama, akikabidhi mikopo hiyo jijini Arusha amesema serikali itaendelea kuwakwamua wanawakekiuchumi, hii inatokana na asilimia kubwa ya utafiti kuonyesha wanawake ndio wengi wanakabiliwa na changamoto zakutaokuwa na ajira .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa huo ni mwendelezo wakuwasidia wananchi wa hali ya chini wasiokopesheka na benki kutokana na uwepo wamasharti magumu hivyo mkopo huo utawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo Marrygoreth Leonard amesema itawainua kutoka hatua moja hadi nyinge na kujikwamua kiuchumi,
wadau waliofanikisha akiwemo Mfanyabiashara Willbard Chambulo, mikopo hiyo wakiahidi kuendelea kuwasaidia wanawake hao ili kupunguza umasikini katika kaya nyingi za wakazi wa jiji la Arusha.
Mikopo hiyo ni sehemu ya marejesho ya zaidi ya milioni mia tatu zilizotolewa walikwa waendelesha bodaboda katika mkoa wa Arusha ambazo wameshazirejesha.

No comments